November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maveterani wakutanishwa bonanza la Michezo kuelekea miaka 60 ya JKT

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewakutanisha wachezaji wa zamani (Maveterani) wa Timu za Majeshi katika Bonanza la michezo ambalo ni moja ya shughuli zinazofanywa na Jeshi hili kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo mnamo Julai 10, 1963.

Akizungumza wakati akifungua Bonanza hilo lililokuwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka,Netball na Vollebal, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa JKT Kanali Issa Mlay amesema katika kuadhimisha miaka 60 ya JKT ,Jeshi hilo lilianza na JKT Marathon ambayo iliwakutanisha wachezaji mashuhuri kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Katika yote hayo pia yanachangia katika kujenga ushirikiano baina ya Jeshi na Wananchi lakini pia hjusaidia katika suala zima la kuimarisha afya.”amesema Mkurugenzi huyo

Kwa upande wake Katibu wa kamati ndogo ya Maadhimisho hayo Kaptein Godwin Ekingo amesema bonanza hilo linashirikisha timu tatu ambazo ni JKT Veterani, Twalipo Vetereni ya  Dar Es saalam na Watumishi Vetereni huku akisema,mshindi wa kwanza na wa pili katika bonanza hilo watapata zawadi siku ya kilele cha maadhimisho hayo.

Kwa upande wa wachezji hao wamelipongeza JKT kwa kuwakumbuka wachezaji wa zamani na kuwakutanisha katika bonanza hilo.

Aidha wamelipongeza Jeshi kwa timu zake kupanda  kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara huku wakisema ni hatua nzuri kwani inasaidia katika suala zima la ajira kwa vijana.

Mpira wa soka umechezwa katika viwanja vya Kilimani eneo la Uzunguni huku Netball na Vollebal zikichezwa katika viwanja Chinangali.