December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Matukio yaliyosisimua katika picha

PICHANI JUU KUSHOTO: Mwanaume aliyevalia mavazi ya ‘Spider-Man’ akiwa amekaa kando ya msafara wa teksi wakati madereva teksi wakiwa wamefanya mgomo juu ya programu tumishi za Uber, Cabify na Didi katika eneo la Angel de la Independencia mjini Mexico City, Mexico juzi. Madereva wanadai kutonufaika kupitia programu hizo. (Picha na REUTERS).

Wachezaji wa Los Angeles Lakers wakisherehekea baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, NBA baada ya ushindi wa pointi 106-93 dhidi ya Miami Heat kwenye mchezo wa sita wa fainali na kufanya ushindi wa jumla 4-2. (Picha na TODAY SPORTS)
Wataalam wa afya wakichukua vipimo vya maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) kwa wananchi mjini Qingdao, Mashariki mwa Jimbo la Shandong nchini China juzi. (Picha na AFP).
Wakazi wa Jimbo la Shan nchini Mnyanmar wakinunua bidhaa kwa wachuuzi kupitia boti zilizotandazwa katika mwambao wa Ziwa Inke juzi ikiwa ni utaratibu uliowekwa ili kuepusha misongamano ambayo inaweza kusababisha maambukizi ya Corona. (Picha na AFP).
Mfanyakazi akishusha boga kubwa kwa ajili ya maonyesho ya maboga makubwa duniani yaliyofanyika mjini Califonia nchini Marekani Oktoba 12, 2020. (Picha na AFP).