December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Muonekano wa sehemu ya Mji wa Kumamura, Kumamoto Prefecture Kusini Magharibi mwa Japan ukionekana umeharibiwa vibaya na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo ilinyesha juzi na kusababisha maafa mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali. (Picha na REUTERS).

Matukio mbalimbali katika picha duniani

Ndugu wakimuombea mwanamke aliyefariki kwa virusi vya Corona (COVID-19) juzi mjini New Delhi, India. Bado wataalam wa afya wanasisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za afya ili kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya Corona. (Picha na REUTERS).
Wanafunzi na mwalimu Shule ya Ban Pa Muad mjini Chiang Mai Kaskazini mwa Thailand wakiwa wamevalia kofia maalum zenye vitenganishi vya nafasi baina ya mwanafunzi na mwanafunzi wakati wakiwa darasani ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19). (Picha na AP).
Watoto wakitumia mpira wa maji juzi kujipooza kutokana na joto kali ambalo limeendelea kurekodiwa mjini Rawalpindi, Pakistan. (Picha na AFP).
Fundi umeme akirekebisha hitilafu zilizobainika katika nyaya za umeme mkubwa kama alivyokutwa juzi mjini Yangon, Myanmar. (Picha na AFP).