Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino kwa ajili ya hafla ya chakula cha mchana iliyowandalia Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
PICHA ZOTE NA IKULU
Baadhi ya Mawaziri wakicheza nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa katika hafla maalumu ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Wasanii wa Kizazi kipya Ali Kiba pamoja na Harmonize wakitoa burudani katika hafla hiyo ya Chakula cha Mchana katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na viongozi wengine wakiweka zege kama kumbukumbu katika ujenzi wa Ofisi mpya za Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Viongozi Wastaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Wajumbe wengine wa Mkutano Mkuu wakicheza mziki katika hafla ya Chakula cha Mchana kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Wasanii wa Kizazi kipya Harmonize, Ali Kiba na Diamond wakiwa wameketi pamoja katika hafla ya chakula hicho cha mchana kwa ajili ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
More Stories
Haya hapa matokeo yote kabisa ya Form Four
Bodi ya NHIF yatakiwa kutatua changamoto za wanachama wake
Rais Samia, Mwinyi ‘mitano tena’ Nchimbi aula