December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Matukio mbalimbali duniani wiki hii – Picha

Mwanamke aliyekutwa amebeba mizigo na mtoto wake akielekea katika moja ya kambi duni iliyopo Faladie mjini Bamako, Mali juzi. (Picha na AFP).
Watu wakiwa katika mstari kuelekea kupokea chakula cha bure kinachotolewa na Serikali mjini Bangkok, Thailand ili kuwapunguzia gharama za maisha wananchi kipindi hiki cha mlipuko wa corona. (Picha na REUTERS)
Afisa wa Jeshi la Polisi nchini Indonesia akinyunyizia dawa pikipiki katika kituo cha ukaguzi kilichopo Surabaya Aprili 28, mwaka huu. Mkakati huu unalenga kudhibiti virusi vya corona katika vyombo vyote vya moto na mizigo. (Picha na AFP).
Baadhi ya maafisa wa Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto nchini Korea Kusini wakishirikiana kuzima moto katika ghala la kuhifadhia bidhaa lililokuwa linateketea juzi mjini Icheon. Katika ajali hiyo zaidi ya watu 38 waliripotiwa kufariki na mamia kujeruhiwa. (Picha na AFP).
Kikosi cha Bandari nchini Ufilipino kikisambamza baadhi ya bidhaa na chakula kwa wananchi waishio katika Pwani ya Manila Bay Aprili 27, mwaka huu, ikiwa ni hatua ya kuwasaidia kumudu maisha kipindi hiki. (Picha na EPA-EFE).MA