January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanaume aliyekutwa amepakia familia yake juzi katika pikipiki kwenda kutafuta hifadhi mjini Mumbai, India baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya na kimbunga Nisarga ambacho kinaelezwa kuwa hatari zaidi nchini humo. (Picha na REUTERS).

Matukio duniani katika picha

Waumini wakiendelea kufanya sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Fatih uliopo mjini Istanbul huku wakiwa wamezingatia miongozo ya kutokaribiana na kuvaa barakoa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19). (Picha na AFP).
Myama kima akipokea zawadi ya embe kutoka kwa msamaria mwema barabarani mjini Hua Hin, Thailand. Kwa sasa wanyama hao wanatajwa kukabiliwa na hali ngumu kutokana na idadi ya watalii ambao awali walikuwa wanawalisha kusitisha safari za kutalii, hali inayochangiwa na mlipuko wa virusi vya corona. (Picha na AFP).
Kikosi kazi maalum nchini Indonesia kikijiandaa kwa ajili ya kwenda kunyunyiza dawa maalum ya kukabiliana na virusi vipya vya corona (COVID-19) kama walivyokutwa juzi karibu na Istiqlal Mosque mjini Jakarta. (Picha na AP).
Mwanaume aliyekutwa akiburuza robota la chupa za plastiki kwa ajili ya kuzirejesha viwandani baada ya kuziokota mitaani eneo la Phumlamqashi mjini Johannesburg, Afrika Kusini juzi. (Picha na AP).