Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mara, Faustine Matiko, ameweka wazi nia ya kuwania Ubunge katika jimbo jipya la Kivule jijini Dar es Salaam, katika uchaguzi mkuu,unaotarajia kufanyika mwaka huu.
Matiko ambaye ni mfugaji wa kuku, amewahi kugombea Ubunge Jimbo la Musoma mkoani Mara mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar- es-Salaam,Matokeo,ametaja vipaumbele vyake endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,ni pamoja na kuanzisha soko kuu la uzalishaji na usambazaji wa mayai ndani na nje ya nchi litakalogharimu zaidi ya bilioni 1.
Amesema,Kivule ni moja ya eneo ambalo linazalisha mayai kwa kiwango kikubwa,hivyo amechukulia kama fursa,hivyo alipata Ubunge ataanza ujenzi wa soko hilo ndani ya siku 100.
“Nitakapochaguliwa moja ya kipaumbele changu kama Mbunge wa Kivule ni kuanzisha soko kuu ambalo litasaidia hata wafanyabiashara kusafirisha kwa urahisi na usalama zaidi mayai,”amesema Matiko.
Pia ameahidi, kushirikiana na viongozi wa Manispaa ya Ilala kuweka mipango thabiti ya ujengaji wa soko hilo ambalo litaweza kuwa mkombozi kwa wakazi wa Kivule pamoja na kuongeza uchumi wa taifa.
Hata hivyo ametaja kipaumbele kingine ni kuhamasisha wanakivule kuendelea kutumia majiko ya gesi kwa ajili ya kuimarisha matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na uboreshwaji wa miundombinu ya barabara.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako