Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),imeanza utekelezaji wa maandalizi ya matengenezo ya dharura ili kuzuia uvujaji wa maji katika maungio ya bomba la inchi 40 na inchi 28 katika mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu.
DAWASA imelazimika kuzima mtambo wa Ruvu Juu kwa saa 24,ili kuruhusu matengenezo hayo na kusababisha maeneo ya Kibaha hadi Kisarawe kukosa huduma ya maji.
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji, Mhandisi Leonard Msenyele, amesema kazi inaendelea kufanyika usiku na mchana na inategemea kukamilika ndani ya muda uliowekwa.
“Wataalam mbalimbali wanaendelea na kazi hii usiku kucha,kuhakikisha inakamilika ndani ya muda uliopangwa na kuwezesha huduma kurejea kwa katika hali yake ya kawaida,” amesema Mhandisi Msenyele.
Mtambo wa Ruvu Juu unahudumia maeneo ya Mlandizi, Kibaha, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisa.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya