Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Mashirikisho ya vyama mbalimbali mkoani Mwanza,yameunga mkono azimio la mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa, la kuwapitisha wagombea Urais na Makamu wa Urais, watakao peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika 2025.
Huku wakieleza sababu za kuunga mkono azimio hilo ni kuridishwa na utekelezaji uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussen Mwinyi.
Viongozi wa mashirikisho hayo wamezungumza katika mkutano wa hadhara wa kuunga mkono wagombea wa Urais mwaka 2025 kwa tiketi ya CCM,uliofan,ofisi za chama hicho Mkoa wa Mwanza.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Wilaya ya Ilemela, Sylvester Nkumillah,amesema Rais Samia, ni mama shupavu na mwenye kuangalia makundi yote na hiyo ndiyo sababu ya kuunga mkono azimio hilo.
“Ndio maana watu wenye ulemavu baada ya kuona jina limepitishwa,wote tulishangilia, kwani aliwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya,wahakikishe watu wenye ulemavu wanapata ofisi zao.Nampogeza Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla ametekeleza azimio hilo na ametupatia ofisi kwa upande wa Wilaya ya Ilemela,”.
Sanjari na hayo Nkumillah,amekataa na kuipinga vikali kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa kundi la watu wenye ulemavu limesahaulika,huku akidai kuwa wanaotoa kauli hizo ni wale wanaotumia nguvu kupora haki zao.
“Julai 17,2017,Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,lilitoa waraka wakiwaelekeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri nchi nzima,kutenga asilimia kwa ajili ya mikopo ya watu wenye ulemavu, pia wanapotenga maeneo ya biashara watenge asilimia 10,kwa ajili ya watu wenye ulemavu, changamoto jambo hilo alifanyiki nchi nzima,amesema na kuongeza.
“Katika mikopo ya asilimia 2, kwa watu wenye walemavu,tulikuwa hatukopeshwi bali tulipewa fedha za majaribio,hivyo fedha za majaribio hazilipwi,napinga kuwa watu wenye ulemavu hatulupi mikopo,kwani tulikuwa tukiomba mkopo wa milioni tano tunapewa milioni moja,na tukiuluza tunajibiwa kuwa hizo ni kwa ajili ya majaribio,”.
Katibu wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania Venatus Anatory,amesema,sababu ya kuunga mkono azimio la mkutano mkuu wa CCM,kwa sababu Rais Samia amewafanyia mambo makubwa ikiwemo kuwapatia ofisi nchi nzima.
“Pia ametupatia ofisi ambayo inatuhudumia machinga mkoani Dodoma,anatutengea fedha kila mwaka kwa ajili ya kuboresha biashara zetu,tupo pamoja mguu kwa mguu ili apate kura za kutosha,”.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda,Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala,amesema ya kutokana na uwekezaji uliofanywa na Dkt.Samia Suluhu Hassan,tangu alipo ingia madarakani wana Mwanza wanayo haki ya kuunga mkono azimio hilo na kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa taarifa pindi zoezi litakapoanza ili waweze kumchagua Rais Samia,katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Masala amesema,kwa kipindi hicho chote Mkoa wa Mwanza umepokea kiasi cha tirioni 5.6, kwa ajili ya kuendeleza,kukamilisha na kumaliza miradi mbalimbali ya ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji Butimba,ambao umekamilika,upanuzi wa chanzo cha maji Capripoint ili kuweza kufikisha huduma katika maeneo ambayo maji hayajafika.
Pia ameboresha katika sekta ya elimu,afya,ujenzi wa vivuko vitando ndani ya Ziwa Victoria ambavyo vinatarajia kukamilika Machi 31, mwaka huu.Pia wanatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Mwanza mjini hadi Usagara.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza,Michael Lushinge, amesema,amewapongeza viongozi wa mashirikisho hayo kwa kuunga mkono na mkutano mkuu wa CCM Taifa,kwa kuwateuwa viongozi hao kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mkuu.
“Kama chama tumefanya mambo makubwa,tumeimarisha Jumuiya zetu,katika zoezi la uandikishaji kama mwaka mmoja tulikuwa na wanachama milioni 3, lakini sasa tumeisha fika wanachama milioni 12.5,”,hivyo mwaka huu uchaguzi mkuu watashinda kwa kishindo,”.
More Stories
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo
Maelfu kunufaika namsaada wa kisheria Katavi
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano