Na Mwandishi wetu
WACHEZAJI wa ridhaa wa Mchezo wa Golf wameshiriki mashindano ya wazi ya TPC yanayoendelea kuchezwa katika viwanja vya kiwanda cha miwa cha TPC moshi Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza leo wakati wa kuanza kwa mashindano hayo Nahodha kwa klabu ya Golf ya TPC,Jaffary Idd amesema Malengo ya mashindano hayo ni kukuza mchezo huo na kuongeza idadi ya wachezaji.
“Tunaendelea kukuza mchezo hatua sio mbaya tuna vijana wengi sana wanacheza,tunaamini baada ya muda mfupi tutakuwa na wachezaji wengi wazuri kwa maslaho ya Taifa,”amesema
Aidha alisema programu ya watoto imekuwana tija na imekuwa kipaumbele na wanatarajia kuendesha mashindano makubwa ili kuendelea kutoa hamasa.
Kwa Upande wake Mchezaji namba moja wa Klabu hiyo,Ally Mcharo amesema matumaini yao makubwa ni kupata ushindi.
Mcharo ambaye kiwango chake cha uchezaji ni zaidi ya fimbo tano amesea baada ya kumaliza mashindano hayo anamatumaini makubwa ya Klabu kumpa fursa zaidi kimataifa .
Naye Mchezaji upande wa timu ya wanawake,Hadija Selemani wa Timu ya Golf Lugalo amesema mchezo ni mgumu ila anaamini watafanya vizuri.
Hadija ni miongoni mwa wachezaji 10 wa Lugalo walioshiriki mashindano hayo sambasamba na wachezaji wengine kutoka Arusha Gymkhana ,Moshi na Kili Golf.
Mashindano hayo ya wazi ni ya siku mbili kwa wachezaji wa ridhaa na wakulipwa yanatarajia kuhitimishwa kesho jumapili huu kwa wachezaji wa kulipa yanatarajia kuhitimishwa leo baada ya kuanza jana.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya