May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashindano ya pili ya kuifadhi Qurani Buyuni yamalizika

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

Mashindano ya kuifadhi Qurani tukufu Buyuni Mtaa wa Nyeburu yamemalizika huku Fatuma Shaibu akiibuka Kidedea kutoka Kigezi kwa kuifadhi juzu kumi.

Mashindano ya pili ya kuifadhi Qurani tukufu yalioandaliwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Nyeburu Hamis Gea, yameshirikisha madarasat za Buyuni zote ambazo washiriki walikuwa kutoka vyuo mbali mbali ambapo leo ilikuwa Fainali yake.

“Mwanafunzi Fatuma Shaibu kutoka Kigezi amekuwa mshindi wa jumla kwa kujinyakulia kitita cha shilingi elfu 70,000/= kutoka kwa mratibu wa Mashindano haya”alisema Gea.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Nyeburu Hamis Gea alisema Mashindano hayo yalianzishwa mwaka 2023 kwa mara ya kwanza mwaka huu ni awamu ya pili yanaendelea kupokea washiriki kila mwaka .

Alisema dhumuni la mashindano hayo katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwaanda watoto katika misingi imara waweze kujua Qurani tukufu na misingi yake .

Aidha Mwenyekiti Gea alisema Mashindano hayo yalizinduliwa Rasmi mwaka 2023 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya ilala Mohamed Msophe na mwaka huu 2024 awamu ya pili ambapo Mwenyekiti Mohamed Msophe ametuma Mwakilishi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala Saabry Abdalah Sharif ndiye alikuwa mgeni rasmi.

Alisema vyuo zaidi ya 30 vilishiriki mashindano hayo kwa mwaka huu mwaka 2025 mashindano hayo yatakuja kwa sura mpya zaidi .

Aliwataka Wazazi kuwajengea watoto misingi bora ya dini yao kwa kuwapeleka madarasa kusoma Qurani tukufu ,watoto wanapojua Qurani tukufu kunawapelekea kufanya vizuri Darasani kitaaluma.