Na Penina Malundo
Mashindano ya Gofu kumuenzi Lina kuanza kurindima tena Aprili 11 Mkoani Morogoro ikiwa ni awamu ya pili ya Mashindano ya Gofu yaliyofanyika Moshi kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Wanawake ya gofu Lina Nkiya kwa kushindana .
Michuano hiyo inayoitwa Lina PG Tour imeandaliwa na familia ya Said Nkya kwa kushirikiana na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) kwa lengo la kumuenzi mchezaji huyo aliyekuwa na mchango mkubwa kwenye timu na TLGU.
Lina alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliopeperusha vyema bendera ya Tanzania mwaka 2011 walipotwaa taji la Afrika Mashariki na Kati katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Dar es Salaam.
Makamu Rais wa TLGU Ayne Magombe amesema mashindano hayo yatafanyika katika mikoa tofauti na hiyo yote ni kuendelea kumuenzi mchezaji huyo kwa kuibua vipaji na kushindana.
“Nategemea kuona ushiriki mkubwa wa wachezaji kama ilivyokuwa Moshi tulipata mwitikio mzuri, hiyo yote tunathamini kile ambacho akifanya Lina enzi za uhai wake alikuwa anapenda sana mchezo huu,”amesema Mume wa Lina Said Nkiya
Amesema sababu ya kuzunguka kufanya utalii wa gofu ni kwa kuwa mke wake huyo aliupenda mchezo huo na kuwasaidia wengi hivyo, wanataka kuendeleza pale walipoishia kwa kusaidia wengine kuinuka.
Amesema kama walivyofanya Moshi kwa kutoa zawadi nzuri wataendeleza kwa watakaofanya vizuri katika mikoa yote watakayoenda na kuwahimiza wachezaji mbalimbali kujitokeza na kujisajili ili kushiriki kwa wingi.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria