November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashindano mpira wa pete daraja la pili kitaifa yazinduliwa

Na George Mwigulu,Timesmajiraonline, Nsimbo.

MBUNGE wa Jimbo la Nsimbo Mkoa wa Katavi, Anna Lupembe amezindua mashindano ya mpira wa pete daraja la pili Kitaifa yanayofanyika katika Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi  kwa muda wa siku kumi ambapo timu mbalimbali za mpira wa pete zimekutana kushiriki mashindano hayo.

Kuletwa kwa mashindano hayo katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo ni kutokana na shirikisho la mpira wa pete nchini kuona nia na mapenzi ya mbunge wa jimbo hilo kwenye masuala ya kimichezo ambapo siku za hivi karibuni ametumia fedha zaidi ya mil.65 kufadhili michezo ya mpira wa miguu kupitia LUPEMBE CUP na kufanya matamasha ya mashindano ya ngoma za asili,muziki wa kizazi kipya na kwaya.

Akizindua mashindano hayo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Nsimbo amesema ujio wa mashindano hayo katika Halmashauri ya Nsimbo nikielelezo cha uwepo wa miundo mbinu ikiwemo viwanja vya kisasa ambavyo vimejengwa na kukidhi kufanyika kwa mashindano hayo ngazi ya taifa.

Mbunge huyo amesema kuwa kupitia mashindano hayo Kufanyika katika mkoa wa Katavi yata utangaza Mkoa na Halmashauri kwa ujumla kupitia michezo hiyo na kuwaomba washiriki wa michezo hiyo kucheza kwa nidhamu ili kumpata Bingwa wa Mpira wa Pete kitaifa wa ligi Daraja la pili anaestahili.

Katika hatua nyingine ameshukuru uongozi wa Chama cha Mpira wa Pete Tanazania CHANNETA kwa kuupa heshima mkoa wa Katavi wa kuwa mwenyenyeji wa mashinadano ya mpira wa pete ngazi ya taifa na kukiomba chama hicho kutembea katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuhamasisha zaidi mchezo huo kwa Vijana.

“Katika siku chache zilizopita tulianzisha ligi katika kata zetu maalufu kama Lupembe CUP nimetoa zawadi kila Kata zawadi kwa makundi mbalimbali yenye thamani ya  zaidi Shilingi Milioni 1 na laki 4 ili kuunga juhudi za Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kukuza michezo’’ anasema Lupembe

Ameeleza kuwa katika kukuza vipaji vya wasanii wa nyimbo za kikazi kipya na Nyimbo za utamaduni ameanzisha mashindano ya utamaduni katika kila kata ili kusaka vipaji na kuviendeleza kwa kuwaunga mkono kwa kutoa zawadi kwa washindi.

‘’Nimeanzisha michezo ya utamaduni nimepita kwenye kata nimeona vikundi mbalimbali vya Vijana wa mziki wa kileo wameimba wamecheza tumeona ngoma za utamaduni mimi kama mbunge nimetoa zawadi kila kata milioni Tatu hadi tano kulingana na ukubwa wa kata hii yote kuunga mkono juhudi za kukuza Sanaa kupitia utamaduni na mpira wa miguu nimetumia zaidi ya Shilingi Miloni 65 kufanikisha michezo hiyo ndani ya jimbo la Nsimbo’’ amebainisaha lupembe

Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Pete Tanzania Dk Devotha Malwa amesema mashindano hayo yatasaidia vikupwa katika kuendeleza mchezo wa Mpira wa Pete kwa kuwapata wachezaji watakao saidia katika mashindano mbalimbali ya kitaifa.

Devotha amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya Viwanja vya Mpira wa Pete wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali ili kuwasaidia kupata miundo mbinu ikiwemo halmashauri za Wilaya kwa kuziomba kujenga Viwanja hivyo.

Nao baadhi ya washiriki wa mashindano hayo,Maria Zachal kutoka timu ya mpira wa pete VETA QUEEN ya Mkoa wa Katavi ameishukuru CHANNETA kwa kuyaleta mashindano hayo muhimu katika mkoa huo.

Maria amesema kuwa timu yao imejianda vema kwa ajili ya kushinda mashindano hayo kwa sababu wanaari nzuri na afya njema ya kushindana ili kupata matokeo mazuri.