December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashindano mchezo wa bao yaandaliwa, washindi kupata zawadi

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

TAASISI ya Tulia trust yenye makao makuu yake mkoani Mbeya inakwenda kufanya mageuzi kwenye mchezo wa bao uliozoeleka kuwa ni wa vijiweni kwa kuandaa mashindano ya mchezo huo huku washindi wakipata zawadi pamoja na kuendeleza vipaji vyao.

Mratibu wa Mashindano ya Tulia Trust Dice Competition, Athumani Kapuya amesema.mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 17 mwaka huu jijini Mbeya lengo likiwa ni kutoa fursa kwa vijana kuonesha umahiri wa vipaji na mshindi wa kwanza mpaka watatu watajinyakulia kitita cha fedha.

Kapuya amesema kuwa mashindano hayo yatahusisha vipengele vinne,ambavyo ni kuimba,kucheza,fashion na kuchekesha.

Amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika mara nne mfululizo kwa lengo la kuibua,kukuza,kuendeleza na kubadili vipaji vya wananchi kuwa ajira na kujinuua kiuchumi kwani washindi watatu kwenye kila Kipengele watapatiwa zawadi nono na fursa mbalimbali za kuendeleza vipaji vyao.

Pia amesema mashindano hayo yatafanyika eneo la viwanja vya Ndege vya zawani (Airport ya zamani)Kata ya Iyela Jijini Mbeya ambapo washiriki watatakiwa kujisajili ili kupata fursa ya kushiriki.”Dhumuni la kuendeleza mchezo wa kete na kuufanya kuwa fursa ya kiuchumi katika jamii “amesema.

Kwa upande wake, Meshack Paul maarufu Nox M msanii wa ucheshaji nchi amempongeza Dkt. Tulia kwa kufungua fursa kwa wananchi wake hususani kwenye michezo ili kuweza kuinua vipaji kwa vijana pamoja na kuendeleza michezo hiyo.