January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashabiki walalamikia utaratibu ‘mbovu’ kuingia kwa Mkapa

Na Yusuph Digossi, TimesMajira Online

MASHABIKI mbalimbali waliojitokeza katika uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga utakaoanza saa 11:00 jioni wamelalamikia utaratibu mbovu wa kuingia uwanjani jambo linalosababisha msongamano mkubwa wa mashabiki.

Baadhi ya mashabiki hao wameuambia Mtandao huu kuwa, utaratibu uliowekwa ni kama umeshindwa kusimamiwa jambo linalofanya baadhi ya mashabiki kujichomeka katika mistari hiyo.