Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ,Hamad Masauni amesema kituo cha Taifa cha ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) nchini kilichopo Mkoani Morogoro kitakuwa ni miongoni mwa taasisi muhimu nchini katika kusaidia Taifa .
Ameyasema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho kilichopo mkoani Morogoro amesema kutokana na miradi mbali mbali ambayo mataifa ya nje yanakuja kuwekeza kupitia biashara hiyo ya Kaboni, biashara hiyo itaweza kusaidia katika kukuza kipato cha wananchi lakini pia kuchangia uchumi wa nchi kwa ujumla.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/3-2-1024x682.jpg)
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ambae alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika ziara hiyo amesema mkoa huo umejipanga kutumia vyema fursa hiyo ili kutekeleza na kutafsiri kwa vitendo maelekezo na maono ya Rais Samia ya kuhakikisha biashara ya Kaboni inakuwa vyenzo vyengine ya kuinua kipato cha wananchi na kuchangia katika maendeleo nchini.
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/2-4-1024x682.jpg)
“Ni fursa muhimu sana kwetu uwepo wa kituo hiki mkoani kwetu ni hatua muhimu sana, kwani vianzio vyote vinavyopelekea biashara hii kufanyika tunavyo kupitia misitu, mifugo na mito tutahakikisha fursa hii inatumika vyema na tija iweze kuonekana kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kupitia rasilimali tulizonazo” Amesema Shaka
More Stories
Wakuu wa nchi wa EAC,SADC watoa maazimio kumaliza mgogoro wa Congo
Wanafunzi wawili waliodaiwa kutekwa wapatikana,watuhumiwa wauwawaÂ
Watumishi Madini waaswa kufanya kazi kwa bidii, kuwa wazalendo