April 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Masauni  afanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya NEMC 

Na Mwandishi wetu, Timesmajira 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Mhandisi Hamad Yusuf Masauni  kwa mujibu wa Kifungu Na.19 (2) (C) cha Sheria ya Usimamizi Mazingira Na. 20 ya Mwaka 2004,amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). 

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Makamu wa Rais, Sarah  Msika amewataja wajumbe hao ni pamoja na Dkt. Abubakar  Rajab,Prof.Hamisi  Malebo,Prof. Theobald  Theodory,Mhandisi Bashir  Mrindoko na Said Habibu Tunda.

Wengine ni Alex  Mgongolwa,Rabia  Hamid na Mhandisi Kemilembe Mutasa ambapo uteuzi wa wajumbe hawa umeanza April 9 , 2025 na utadumu kwa  muda wa miaka mitatu.

Uteuzi huu umekuja kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kumteua Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),