*Ni kufuatia kifo cha Katibu UWT Mbeya
*Mtoto mmoja wa marehemu kusomeshwa hadi chuo kikuu
Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
MBUNGE wa Jimbo la Lupa wilayani Chunya ,Masache Kasaka,amesema kuwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Katibu UWT Mkoa wa Mbeya ,Lucia Sulle,Chama Cha Mapinduzi (CCM),wamepoteza mtu muhimu hususani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Marehemu Lucia ni miongoni mwa watu walipata ajali Februari 25 mwaka ,baada ya gari la Serikali lililokuwa kwenye msafara wa kiongozi wa CCM kupata ajali katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya.Ambaye amefariki Aprili Mosi mwaka huu katika Hosptali ya Rufaa Kanda akipatiwa matibabu.

Masache amezungumza hayo Aprili 2,2025 kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Mbeya wakati wa kuaga mwili wa Katibu huyo,uwanja wa Uhindini jijini Mbeya, ambapo amesema,marehemu enzi za uhai wake alikuwa mchapa kazi kama Wabunge wamemfaidi sana kwa namna alivyokuwa akisimamia haki.
Sanjari na hayo amewahimiz Wana-CCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya kumuenzi marehemu Lucia huku akisisitiza kuwa pengo lake halitazibika kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Kwa upande wake ,Mbunge wa Jimbo la Rungwe,Athony Mwantona amejitolewa kusomesha mtoto mmoja wa marehemu kuanzia elimu aliyonayo mpaka chuo kikuu ili atimize ndoto yake.

Naye,Mbunge viti maalum Mkoa wa Mbeya,Suma Fyandomo, amesema,”Binafsi tumekuwa bega kwa bega ,lakini kipekee nimshukuru Mbunge wa Mbeya Mjini,Dkt.Tulia Ackson amekuwa mstari wa mbele kufuatilia maendeleo ya afya ya marehemu mpaka umauti unamkuta,”amesema.
More Stories
Apps and Girls, Yas Waadhimisha Mahafali Wahitimu wa Jovia 2025
Benki ya Exim yaboresha uchukuaji mikopo kwa watumishi wa umma
Ally Kamwe ashikiliwa na Jeshi la Polisi Tabora.