November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maryprisca ampongeza Mwenyekiti UWT Taifa Mary Chatanda

Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya

MBUNGE wa vitimaalum mkoa wa Mbeya na Naibu waziri wa maji Mhandisi , Maryprisca ampempongeza Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda kwa kuchaguliwa kwake kuongoza umoja huo na kwamba wanawake wa mkoa huo wanamuunga mkono na kuahidi kumpa ushirikiano katika majukumu yake.

Mhandisi Mahundi amesema hayo jana wakati wa maandamamo ya kumpongeza makubwa ya kumpongeza Mwenyekiti UWT taifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya yaliyowashirikisha wanawake kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali .

“Mwenyekiti wetu Taifa ni mama shupavu katika uongozi na wanawake wa Mkoa wa Mbeya tunamuunga mkono na tunaahidi kumpa Ushirikiano nyakati zote mawio na machweo kwani tunaamini sisi wanawake atatuvusha katika maendeleo pamoja na kusimama na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan”amesema Naibu waziri wa Maji Mhandisi Mahundi.

Akiongoza maandamano hayo ambayo yaliyoanzia eneo la Mafiati Mataa na kuhitimishwa katika ukumbi wa Tughimbe ambako lilifanyika Kongamano kubwa la zaidi ya wanawake 500 kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya ambazo ni Kyela, Rungwe, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Mbarali na Chunya Mhandisi Mahundi amesema kuwa wanawake wana imani kubwa na Mwenyekiti na kwamba wanawake ni jeshi kubwa ambalo litahakikisha linampa ushirikiano mkubwa utendaji wake wa kazi .

Akitoa tamko la Pongezi hizo mbele ya mgeni rasmi Dkt.Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kumuunga mkono na kumpa tabasamu zaidi kutokana na mambo mazuri yatakayofanywa na Mwenyekiti wao Mary Chatanda.

Mary Mbwilo ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya mbarali amesema kuwa katika kumpa ushirikiano watahakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na kumpa ushirikiano mwenyekiti UWT taifa .

“Tumemchagua Mary Chatanda hatujakosea kabisa sisi kama Jumuiya ,huyu ni mwanamke mpambanaji kwetu kwasasa jumuiya yetu itazidi kusonga mbele zaidi na zaidi ,wanawake tunapata nguvu ya kujituma kumpa ushirikiano Mwenyekiti wetu pamoja na Naibu waziri wa maji , Mhandisi Maryprisca Mahundi mwanamke mchapa kazi mpambanaji na anayejali wanawake wenye vipato vya chini “amesema Mwenyekiti huyo.

Katika Pongezi hizo Mheshimiwa Maryprisca alienda mbele zaidi kama kawaida yake ya Moyo wa shukrani akisema wanawake wa Tanzania wanayo bahati ya kupata viongozi wazuri kuanzia ngazi ya juu ambayo anaongoza Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbali na Pongezi hizo, aliwasihi wanawake kuendelea kupendana na kufanya kazi kwa kusaidiana maana wanawake ndiyo waatamiaji wa kwanza wa familia, hivyo suala la Mwanamke kumiliki uchumi imara ni jambo linalopaswa kupewa tabasamu.