November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Martini Kadinda awang’ata sikio wanawamke wajasiriamali kisiwani Zanzibari

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MBUNIFU nguli wa mavazi nchin Martin Kadinda amewataka wanawake wajasiria mali na vijana wa wilaya ya Magharibi ‘A’, kisiwani Zanzibari, kutumia utofauti alio nao binafsi kuboresha biashara yake.

Maritni ni miongoni mwa wabunifu wajasiriamali walio fanikiwa na kutambulisha taifa katika sekta ya mavazi na kujitwalia tuzo sita za kimataifa.

Akizungumza na wanawake wajasiriamali, katika kilele cha mafunzo ya Mwanamke Fanikisha, amesema kila mtu ameubwa na utofauti wake ni vizuri kutumia utofauti huo kutofautisha biashara yake.

“Binadamu wote ni sawa ila kila mmoja ameubwa na utofauti wake tunaweza kufanya biashara moja ila ukaitofautisha na nyengine kulingana na utofauti ulio nao binafsi ikavutia wateja wengi kwa sababu kila mtu ana kitu kinachomvutia na kukipenda,” anasema Martin Kadinda.

Aliongeza kwa kutoa mfano wote mnaweza kukaanga mihogo mmoja akaweka chachandu ya mbilimbi mwengine akaweka ya embe hapo tayari mmesha tofautisha biashara zenu kila mmoja atakuwa na wateja wake.

Aidha alisema Zanzibar ni kisiwa ambacho kina frusa nyingi za biashara hasa kwa wanawake kwa sababu kuna wageni wa kitalii wengi tofauti na Tanzania Bara.

“Tunapaswa kutumia frusa ya wageni kutoka nchi tofauti kujikwamua kwa kubuni biashara ambazo zitawavuta zaidi watalii niombe serekali kuandaa tamasha kama hili ambalo litawaleta wakufunzi wengi kuja kutoa elimu kwa wanawake wa Zanzibari.”

Semina ya Mwanamke Fanikisha, imefanyika kwa wiki moja ili andaliwa na mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, kwa wanawake na vijana ili kuboresha biashara zao na kujikwamua katika wimbi la umasikini na utegemezi.