January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Martin Kadinda kutinga na Escapade collection mbugani

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mbunifu nguli wa mavazi hapa nchini Martin Kadinda, anatarajiwa kutambulisha collection mpya ya Escapede, katika onyesho la ubunifu wa mavazi lenye dhima ya safari mkoani Manyara katika hoteli ya Mawe mawe Januari 29.

Hii itakuwa ni onyesho lake la kwanza kwa mwaka huu kushiriki hapa nchin mara ya mwisho alitambusha collection ya Vanguard, katika tamasha la Swahaili Fashion Week 2020.

Akizungumza na ukurasa huu amesema dhumuni la Escapade collection ni kushawishi watanzania kufanya utalii wa ndani wakienda katika mavazi yanayo kwenda na wakati.

“Tanzania tuna vivutio vingi ndani ya miaka miaka miwili tumepata muamko mzuri wa kutembelea vivutio vyetu ila wengi wamekuwa wakipata shida katika upande wa mavazi ndio maana nimebuni Escapade collection, kwa ajili ya kuleta umaridadu wakati wa safari za utalii wa ndani,” anasema Martin Kadinda.

Aliongeza kuwa kabla ya onyesho hilo kesho atashiriki kuuza vifaa mbalimbali alivyo tengeneza vinavyo tumika katika safari za utalii katika mnada utakaofanyika katika hoteli ya Mawe mawe.