Na Yusuph Digossi, TimesMajira Online, Dar es Salaam
MBUNIFU wa mitindo hapa nchini Martin Kadinda anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu (Chief Jaji) wa shindano la Miss Sua mwishoni mwa mwezi huu, litakalofanyika katika hoteli ya Cate Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili Waziri wa michezo katika chuo hicho Kanoni Japhet, amesema fainali hizo zitafanyika sambamba na utoaji tuzo kwa wanafunzi katika vipengele mbalimbali.
“Tunatarajia kufanya fainali ya Miss Sua ambapo Jaji Mkuu atakuwa mbunifu Martin Kadinda, kutokana na ukongwe alio nao katika tasnia hii ya urembo, lakini pia tutatoa tuzo mbalimbali kwa wanachuo ambao wamefanya vizuri katika sekta tofauti,” amesema Japhet.
Kwa upande wake Martin Kadinda amesema, huu ni muda muafaka kwa washiriki wa shindano hilo kufanya mazoezi kwa bidii ili kupata matokeo mazuri.
“Sua ni moja ya chuo kinachofanya vizuri katika tasnia mbalimbali, huu ni wakati mzuri kwao kuziishi ndoto zao kupitia vipaji na sanaa,” amesema Martin Kadinda.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA