January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kivutio kimojawapo kinachopatikana katika mbuga mbalimbali nchini. Picha na Imma Matukio

Mapendekezo ya kuinusuru sekta ya utalii yatolewa

MADRID, Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UNWTO) limetoa mapendekezo ya kusaidia sekta ya utalii wakati huu ambapo ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) umetikisa sekta hiyo kote duniani.

Mapendekezo hayo ni sehemu ya kwanza ya matokeo ya vikao ya kamati ya kimataifa ya utalii iliyoundwa kushughulkia janga la sasa, ikijumuisha wawakilishi kutoka sekta ya utalii duniani pamoja na Umoja wa Mataifa.

Taarifa ya UNWTO iliyochapishwa katika tovuti yake inasema kuwa, ìKwa kutambua kuwa sekta ya utalii ni moja ya sekta zilizoathiriwa zaidi duniani kutokana na janga la Corona, mapendekezo yanalenga kusaidia serikali, sekta ya binasi na jamii ya kimataifa kukabiliana na dharura isiyo ya kawaida ya kijamii na kiuchumi ambayo ni COVID-19,”alisema.

Mapendekezo hayo yako 23, lakini yamegawanywa katika sehemu kuu tatu ambazo ni mosi kushughulikia janga huku athari zikipunguzwa.

Mapendekezo muhimu yanataka watu waendelee kutunza ajira zao, kusaidia waliojiajiri, kuhakikisha kuna fedha au ukwasi, kupitia upya kodi, kuhusiana na kutunza kazi, kusaidia wafanyikazi waliojiajiri, kuhakikisha ukwasi, kukuza ustadi wa ujuzi na kufanya mapitio ya kodi, gharama na kanuni zinazohusiana na utalii.

Aidha,mapendekezo haya yamezingatia hali ya sasa ya mdororo wa kiuchumi huku pendekezo la pili likiwa ni kutenga mafungu ya fedha ili kuchochea ukwamukaji.

Orodha hiyo ya mapendekezo inasisitiza umuhimu wa kutoa kichocheo cha kifedha, pamoja na sera nzuri za ushuru, kuondoa vizuizi vya kusafiri mara tu dharura ya kiafya inaporuhusu, kukuza uhamasishaji wa visa, kukuza uuzaji na ujasiri wa watumiaji, ili kuharakisha kuimarika.

Mapendekezo hayo pia yanataka utalii uwekwe katikati ya sera za kitaifa za kuimarisha na mipango.

Pendekezo la tatu ni kujiandaa kwa ajili ya kesho, wanasisitiza uwezo wa kipekee wa utalii wa kuongoza ukuaji wa ndani na kitaifa na kimataifa ambapo mapendekezo yanataka msisitizo mkubwa kuwekwa kwenye mchango wa sekta hiyo kwenye ajenda 2030 au malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na kujenga uwiano kutokana na mafunzo yaliyopatikana na janga la sasa.

Mapendekezo hayo yanataka serikali na watendaji wa sekta binafsi kuwa na mipango ya utayari na kutumia fursa hii kugeukia uchumi wa mzunguko.

Akizungumzia mapendekezo hayo, Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvili alisema,mapendekezo haya mahususi yanapatia nchi orodha ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kusaidia sekta yetu kuendeleza kazi na kusaidia kampuni zilizo hatarini kwa wakati huu.

“Kuzuia athari za ajira na ukwasi, kulinda walio hatarini zaidi na kujiandaa kukwamuka tena, mambo haya yote lazima yawe vipaumbele vyetu muhimu,”alisema.

Aidha,nyaraka yenye mapendekeo hayo itakuwa ikifanyiwa marekebisho kila wakati kuligana na mwelekeo wa janga la COVID-19 na ukweli na uhalisia katika kila nchi duniani.