Na Penina Malundo,Timesmajira
Maonesho na Tuzo za Mitindo za Swahili 2025 (Swahili fashion week) , yaliyochini ya Jukwaa la wabunifu wa mitindo alimaarufu Swahili Fashion Week and Award yanatarajia kuanza rasmi Desemba 5 hadi 7 mwaka huu katika ukumbi wa Parthenon Hall Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Mwanzilishi na Mmiliki wa Swahili Fashion Week ,Mustafa Hassanali alisema katika maonesho hayo takribani wabunifu wa mitindo zaidi ya 50 kutoka Tanzania ,Kenya,Italia,Afrika Kusini,Trinidad na Tobago wanatarajia kuonesha utofauti na ubunifu wao.

Amesema Swahili fashion ni tukio kubwa zaidi ambao ufanyika kila mwaka kwa nchi ya Afrika Mashariki na Kati na uwakutanisha wabunifu kutoka mataifa yanayozungumza kiswahili na zaidi kuonyesha kazi zao,kukuza ubunifu na kuunganishwa na tasnia ya kimataifa ya mitindo.
“Dira yetu daima imekuwa kuinua mitindo ya Afrika hadi viwango vya kimataifa huku tukienzi utambulisho wetu wa kipekee wa kitamaduni,Tunapokumbana la utamaduni bali pia ni mpaka wa ubunifu,”alisema.
Hassanali amesema sherehe hizo zitatambua mafanikio bora kupitia vipengele 29 za tuzo,ikiwatunuku watu binafsi na chapa zilizotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa tasnia ya mitindo ya Afrika.

“Mchakato wa upigaji kura unasimamiwa kwa uwazi na Nexia Tanzania,kuhakikisha uadilifu na uaminifu katika kuwatambua bora kwenye tasnia,”amesema.
Amesema kwa mwaka huu miongoni wa kipengele walichoongeza ni pamoja na kipengele cha Mwanamitindo mbunifu chipukizi na Tuzo ya mwaka huu ni ya kipekee tofauti na za miaka ya nyuma.
Kwa upande wake Afisa Masoko kutoka Hoteli ya Onomo ambaye ni miongoni mwa wadhamini wa maonesho hayo,Philemon Mwakanyamale ameipongeza Jukwaa hilo kwa kuendelea kufanya vizuri katika kuboresha ubunifu wa wanamitendo.
Naye Fauziat Taru kutoka Shirika la Action for Ocean linaloshughulika na Mazingira ya Bahari,amesema wamevutiwa kuwa miongoni mwa wafadhili wa maonesho hayo kutoka na kauli mbiu yao inayolenga masuala ya utunzaji wa mazingira.
Wadhamini wengine waliodhamini maonesho hayo ni pamoja na Doris Mollel Foundation,Ubalozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania,Ubalozi wa Italia nchini Tanzania na wengine wengi.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako