December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maonesho ya 46 ya biashara Sabasaba kufunguliwa rasmi kesho

Na Mwandishi Wetu,timesmajira,Online

KATIBU Mtendaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA), Wamkele Mene anatarajiwa kufungua maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara (DITF) kesho jijini Dar esSalaam.

Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashantu Kijaji alipotembelea katika viwanja vinapofanyika maonesho hayo maarufu kama sabasaba yaliyoanza Juni 28, mwaka huu.

Amesema Septemba,  mwaka jana Bunge lilipitisha mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika na Januari, mwaka huu ilipelekwa taarifa ya kuonesha utayari wa Tanzania kuingia katika eneo hilo la biashara.

“Kawaida wananchi walizoea maonesho yanazinduliwa na kiongozi wa nchi lakini mwaka huu itakuwa ni tofauti, Rais wetu Samia Suluhu Hassan alitoa fursa kwa sisi Watanzania kumkaribisha Katibu Mtendaji huyu na haya ni matokeo ya sisi kuingia huko katika mashirikiano,” amesema Dk Kijaji.

Amewataka wafanyabiashara waanze kuzalisha biashara kwaajilu ya soko la Afrika na sio Tanzania pekee.

Aidha amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa maonesho hayo ambayo amesema kwa mwaka huu yamefana kwa asilimia 97.

“Tujitokeze kwa wingi kuja kumsikiliza mgeni wetu rasmi ambaye atatuekeza fursa mbalimbali zilizopo katika soko hilo ili tuweze kuzitumia kwani tumerahisishiwa,” ameongeza