Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
MTENDAJI Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse, amesema kuwa, Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba ni fursa ya kunadi fursa zinazopatikana katika Sekta ya Madini
Mwasse, amesema hayo, Leo Julai 03, 2024 alipotembelea na kukagua Banda la Wizara ya Madini sambamba na Taasisi zake katika Maonesho hayo ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa zipo fursa nyingi katika Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na Uwekezaji katika Utafiti na Uchimbaji wa Madini sambamba na fursa za utoaji huduma katika maeneo mbalimbali ambayo kuna miradi ya madini ikiwemo vyakula na usafiri.
Ametoa rai kwa wawekezaji na wananchi kutembelea mabanda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake ili wapate kujifunza fursa zilizopo katika Sekta sambamba na kujifunza kuhusu mnyororo mzima wa shughuli za uchimbaji madini.
Wizara ya Madini na Taasisi zake ikiwemo STAMICO, Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST),Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) kwa pamoja wanashiriki katika Maonesho hayo.
Aidha, Rais wa Msumbiji Mhe. Felipe Nyusi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Hafla ya Ufunguzi wa Maonesho hayo leo Julai 3, 2024 akiambatana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku Mkuu huyo wa nchi ya Msumbiji yuko nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku 4.
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi