Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam.
WATEJA wa vinywaji vya Kampuni ya Serengeti Breweries, wemeendelea kuneemeka kwa kujipatia zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na pesa taslimu hadi Mil.5.
Kufuatia promosheni ya “Maokoto Ndani ya Kizibo”, iliyozinduliwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na kampuni hiyo, ambayo inamtaka mteja wa vinywaji vyake, kuingiza tarakimu zilizo ndani ya kizibo kupitia simu yake, ili aweze kujipatia bahati ya kushinda, ambapo kati ya vinywaji hivyo ni pamoja na Serengeti Lite, Serengeti Lager, Pulsner Lager, Guineas Smooth, na Smirnoff.
Mwakilishi wa kampuni ya Bia ya Serengeti, Karolina Mwamaso, hivi karibuni wakati akikabidhi Hundi ya mfano wa Sh. 500,000 kwa mshindi wa maokoto ndani ya kizibo, Mhina Said wa Jijini Mbeya, amewataka wateja kutumia fursa hiyo ya kujipatia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi ya pesa, ili kuweza kujiongezea kipato.
Aidha kwa upande wake, Mwakilishi wa mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries, Wilaya ya Kilosa, Shomari Mohamed wakati akikabidhi mfano wa hundi kwa mashindi wa wa promosheni hiyo, Ally Seed, kutoka Mkoa wa Morogoro, amewataka watu kutokata tamaa na kudai kuwa zawadi bado zipo nyingi watu waendelee kutumia fursa hiyo.
Mmoja wa washindi katika promosheni hiyo inayoendelea, Christina Godfrey, Mkazi wa Nyegezi Mwanza, amewashauri watumiaji wa vinywaji hivyo kuchangamkia promosheni hiyo, huku akidai kuwa, pesa hiyo aliyoipata itaenda kumsaidia kukuza mtaji wa biashara yake anayoifanya pamoja na kumsaidia kuendesha familia yake.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi