Na Rose Itono,TimesMajira,Online,Dar
SERIKALI imesema haitawavumilia Maofisa Ustawi wa Jamii watakaozithibitisha kaya za watu wenye ulemavu zisizo na sifa kwenye mpango wa kupata ruzuku kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizindua zoezi la kuthibitisha watu wenye ulemavu watakaopata ruzuku kutoka TASAF Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu Ikulu, Dkt Moses Kusiluka amesema mpango huu umelenga kuziinua kiuchumi kaya masikini zilizo ndani ya mpango wa TASAF
Amewataka Maofisa Ustawi wa Jamii kufanya kazi ya kuzithibitisha kaya hizo kwa weledi ili kutimiza azma ya serikali.
‘Hatua ya TASAF kuanza kutoa ruzuku kwa kaya za watu wenye ulemavu waliopo ndani ya mpango inaridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ukiwemo wa haki sawa kwa watu sambamba na mikataba ya Tanzania yenye sera zenye lengo la kushughulikia watu wenye ulemavu,” amesema Dkt. Kusiluka.
Ameongeza kuwa pamoja na kazi ya kuzithibitisha kaya wanayokwenda kuianza hivi karibuni baada ya kumaliza mafunzo yao pia wakatumie muda huo kama fursa ya kuisaidia Serikali kujua mambo mapya ili iweze kuyafanyia kazi zake kikamilifu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Godwin Mkisi amesema zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Septemba ili kuziwezesha kaya kupata ruzuku
Amesema takwimu za awali zinaonesha kuna idadi ya kaya 196,372 zenye walemavu, lakini kwa kuwa ulemavu umegawanywa kwenye makundi kundi, lo TASAF itaanza na lile lenye walemavu wa juu sana na walemavu wa juu.
Mkisi amesema kaya zenye walemavu wa kati na wale wa chini wataguswa na zoezi hilo hapo baadaye kadri serikali inapoendelea kupata fedha.
“Lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar ni kuxofikia kaya zote zenye walemavu lakini kwa kuanzia itaanza na makundi hayo mawili lile la walemavu wa juu sana na wale wa juu,” amesema Mkisi.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ernest Kimaya, ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa hatua hiyo na kuahidi kushirikiana mayo kwenye hatua zote ili kuwezesha umasikini ndani ya kaya zilizo kwenye mpango huo kuondoka.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati