March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maofisa Maendeleo,Asasi wasaidia kupunguza ukatili katika jamii

‎Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Nkasi

Imeelezwa kuwa uwepo wa Maofisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata,kamati za kupambana na ukatili na asasi za kiraia kumesaidia kupunguza vitendo vya ukatili katika jamii.

‎Hayo yamebainishwa kupitia vikao vya MTAKUWWA vilivyoketi katika Kata za Majengo, Kirando na Isale vilivyofadhiliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali Kituo cha Sheria na Ustawi wa Jamii Namanyere (SHEUJANA),cha kupata tathimini juu ukatili kati ya wanawake na watoto.


‎Mkurugenzi wa SHEUJANA, Godfrey Ntangare, amesema, mila na desturi za jamii zimekuwa na nafasi ya kutekeleza vitendo vya ukatili lakini elimu inayoendelea na kusimamia na kamati za MTAKUWWA zimesaidia kwa kiasi kikubwa jamii kuelimika na kupunguza vitendo hivyo.

‎Amesema vitendo vingi vya ukatili vinatokana na elimu duni waliyonayo jamii lakini kutokana na mikakati ya mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kushirikiana na serikali kutoa elimu, mafanikio yanaonekana hivyo nguvu zaidi iongezwe ya utoaji elimu.



‎MTAKUWWA ni pango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na kamati zake ni moja ya nyenzo muhimu katika kutoa elimu na kukabiliana moja kwa moja dhidi ya vitendo hivyo kwa kushirikiana na vyombo vya dola.