Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Manispaa Tabora limepitisha makisio ya bajeti ya mapato na matumizi ya sh bil 47.18 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kufanikisha utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi.
Akiwasilisha bajeti hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt Peter Nyanja, Afisa Mipango wa Manispaa hiyo Nelson Mwankina alisema kiasi hicho kitatokana na fedha za mapato ya ndani, ruzuku ya serikali kuu na michango ya wahisani.
Alisema kati ya fedha hizo sh bil 28.7 ni ruzuku ya mishahara kutoka serikali kuu, sh mil 955.6 ni ruzuku ya matumizi ya kawaida kutoka serikali kuu na sh bil 2.8 ni fedha za matumizi ya kawaida kutoka kwenye mapato ya ndani.
Aliongeza kuwa kiasi cha sh bil 14.2 ni fedha za miradi ya maendeleo ambapo bil 4.2 zitatokana na mapato ya ndani ya halmashauri na bil 6.5 ni ruzuku ya serikali kuu kwa fedha za ndani huku bil 3.3 zikiwa ruzuku ya serikali kuu kutoka kwa wahisani wa nje ikiwemo mapato fungwa sh mil 357.7.
Mwankina alisema halmashauri imekadiria kukusanya sh bil 7.5 kutoka katika mapato yake ya ndani sawa na ongezeko la asilimia 34.4 la makisio ya mwaka jana, mapato yasiyofungwa ni sh bil 71.16 na mapato fungwa ni mil 357.7.
Alibainisha makusanyo ya halmashauri kwa vyanzo vilivyoongezeka kuwa ni sh mil 992 za ushuru wa huduma ambapo mwaka jana ilikuwa sh mil 800, ushuru wa kituo cha mabasi sh mil 307 na ushuru wa nyumba za kulala wageni sh mil 188.5.
Vyanzo vingine ni ushuru wa maegesho sh mil 293.8 ambayo ni sawa na ongezeko la sh mil198, ada ya vibali vya ujenzi sh mil 45.3, ushuru wa madini sh mil 759.6 tofauti na sh mil 29 za mwaka jana na ushuru wa vyoo sh mil 344.8.
Alitaja vyanzo vingine kuwa ni uuzaji viwanja ambapo wanatarajia kukusanya kiasi cha sh mil 600 sawa na ongezeko la sh mil 373 za mapato ya mwaka jana na kodi ya pango kiasi cha sh mil 506.7 ambacho ni pungufu ya sh bil 1.2 za mwaka jana kutokana na kuvunjwa kwa baadhi ya mabanda kupisha ujenzi wa soko jipya.
Mstahiki Meya wa manispaa hiyo Ramadhan Kapela alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa anazofanya ikiwemo kuhakikisha miradi yote iliyopangwa na halmashauri inapewa feha ili kutekelezwa inapewa fedha za kutosha na kuanza halmashauri ina kuwezesha halmashauri hiyo kupata asilimia 100 ya makisio ya bajeti yao ya mwaka tanguliza mbele maslahi ya wananchi bajeti .
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini