January 31, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Manispaa ya Shinyanga yaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza kwa 99%

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga katika zoezi la uandikishaji wa wanafunzi darasa la kwaza, imeweza kuandikisha jumla ya wanafunzi 5,233 sawa na asilimia 99 huku makadilio ikiwa ni kuandikisha wanafunzi 5,288 kwa mwaka wa masomo 2025 wakitakiwa kuandikishwa.

Hayo yamebainishwa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Charles Luchagula wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, kwenye kikao kazi maalumu cha uwasilishaji wa udahili na uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali, darasa la kwanza na kidato cha Kwanza.

Kikao kilichofanyika leo Januari 30, 2025 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maafisa Elimu kata, Watendaji wa Kata, mitaa na vijiji pamoja na afisa utumishi kutoka manispaa ya shinyanga.

“Kwa mwaka wa masomo 2025 tumeandikisha Jumla ya wanafunzi wa darasa la kwanza 5,233 sawa 99% huku makadilio yakiwa ni kuandikisha wanafunzi 5,288 kwa mwaka huu, darasa la awali tumefanikiwa kuandikisha wanafunzi 4,2512 sawa na 72% idadi ikihitajika 5,936, huku Jumla ya wanafunzi 3,238 sawa na asilimia 73.4 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wameripoti huku makadilio yakiwa kuripoti wanafunzi 4,409”. Amesema, Luchagula

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro ameupongeza uongozi wa Manispaa kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Manispaa Kuhakikisha Watoto hawazagai mtaani na kuwafanya wapate haki yao ya elimu, huku akiwataka kuongeza juhudi zaidi ya kuwasaka ambao hawajaripoti shule ikiwa nia pamoja na kuwachukulia hatua kali kwa wazazi wa Watoto hao.

“Nikweli jitihada kubwa mmeifanya Kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu, nipende kipongeza tu manispaa hii kwa jitihada hizo, lakini niwatake muongeze kasi zaidi Kuhakikisha mnafikia 100%, kwani Wilaya ninayoiongoza mimi lazima watoto tuandikishe kwa asilimia 100% lengo Kuhakikisha watoto hawazagai mtaani, hususani walio na umri wa kuanza darasa la kwanza kwa uratibu mzuri na usimamizi wa wanafunzi wa Darasa la kwanza, awali na kidato cha kwanza”. Amesema Wakili Mtatiro