December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Manchester yakubali kichapo

Klabu ya Manchester United imekubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali Europa League Dhidi ya Sevilla. Bruno Fernandes alikuwa wa kwanza kuipa Manchester United bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati dakika ya 9 lakini Suso alisawazisha bao hilo dakika ya 26 na De Jong kufunga bao la ushindi dakika ya 78.

Manchester United kwa msimu huu imecheza nusu fainali tatu kuanzia ile ya Carabao Cup ambapo waliondolewa na Manchester City kwa jumla ya mabao 3-2 lakini pia waliondolewa nusu fainali na Chelsea kwa kipigo cha mabao 3-1 na hapo jana walikamilisha kipigo cha tatu kwenye nusu fainali dhidi ya Sevilla.

Kwa mara ya kwanza Manchhester United inamaliza misimu mitatu bila kutwaa kombe lolote kubwa. Sevilla wao wameshatinga Nusu fainali wakimsubiri mshindi kati ya Sharktar Donestik au Inter Millan