December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Manara apewa ubalozi Bayport

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Wachezaji wa mpira wa miguu wametakiwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii hasa katika kufanya mazuri ambayo yatasaidia kupunguza makali ya maisha na kuweza kuisaidia jamii kwa ujumla

Hayo ameyasema leo (Julai 27, 2022) Haji Manara wakati akisaini Mkataba kuwa Balozi wa Taasisi inayotoa mikopo kwa watumishi wa Umma (Bayport) huku wakizindua kampeni yao ya kupata mkopo kidigitali iitwayo ‘Ndiooo kopa Digito’

Manara amesema mpira wa miguu Wameutangaza zaidi na kupeleka kuufanya kuwa biashara kiasi cha kwamba taasisi mbalimbali zinaona umuhimu kushirikisha Watu wa michezo hususani mpira wa miguu katika mambo yao na kuingia nao mikataba

“Tumeweza kuupeleka mpira wa miguu kuwa ni biashara kubwa na kuutangaza kiasi cha kwamba taasisi tofauti tofauti sasa zinaona umuhimu kushirikisha Watu wa michezo hususani mpira wa miguu katika mambo yao na kuingia nao mikataba tofauti tofauti ni heshima kubwa sana kwa mpira wa miguu”

Aidha Manara amesema tangu kuanzishwa kwake taasisi hiyo ya kifedha hadi sasa wamejifunza mengi ikiwemo umuhimu wa muda na gharama kwenye maisha ya Tanzania hivyo wameamua kuja na Mkopo kwa watumishi hao ambapo mtumishi wa serikali ataweza kukopa kwa njia ya kidigitali;

“Sisi Bayport ni wahasisi wa huduma ya kutoa mikopo kidigitali ambapo mtumishi wa umma anapotaka mkopo anauwezo wa kupiga simu na kupata mkopo hapohapo pia Mtumishi wa umma anaweza akawa nyumbani akabinyeza 15049# na kuweza kukopa hapohapo hayo tunayafanya ili kurahisisha muda”

Manara amewaahidi Bayport kufanya kazi nao kwa ukubwa na kutimiza yale matarajio yao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano katika kipindi chote cha mkataba lakini pia ujumbe ambao wanautaka ufike kuweza kufika vile ambavyo zaidi ya matarajio yao.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo Cha uendeshaji Bayport financial services Nderingo Materu, amesema Taasisi hiyo imefanikiwa kudumu kwa miaka 16 hadi sasa ambapo hutoa mikopo yenye riba nafuu kwa mteja na ili kuepusha usumbufu kwa mteja kwa sasa mteja anapata mkopo kwa njia ya kidigitali bila kuwa na viambatanisho vyovyote Mkononi;

“Mtumishi wa serikali kwa sasa anaweza kujipatia mkopo wake hata akiwa nyumbani ambapo mtumishi hatohitajika kuwa na kiambatanisho chochote zaidi ni kuwasiliana na huduma kwa wateja kutoka kwetu na kupata maelekezo ili kupata mkopo huo hapohapo”

Materu aliwataka watumishi wote wa Serikali kuweza kuchukua mikopo kutoka kwao kwani husaidia kurahisisha maisha na kuondoka makali ya maisha