January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Man City yamtolea nje Griezmann

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester City hawana nia ya kumsajili Antoine Griezmann ambaye alitaka kurithi mikoba ya Aguero kwa kile anachodai bado klabu yao haina bajeti ya kutosha.

Hata hivyo, Uamuzi wa Pep Guardiola kutompa Aguero mkataba mpya

mwishoni mwa msimu uliopita kumemwacha mshambuliaji Gabriel Yesu pekee

kutambuliwa kama mshambuliaji mwandamizi kwenye klabu hiyo.

Griezmann, mwenye umri wa miaka 30 raia wa Mfaransa ameshindwa kutekeleza matarajio

tangu kuwasili Camp Nou kutoka Atletico Madrid mnamo 2019

huku akifunga mabao 22 tu katika michezo 71 ya La Liga.

Mbali na hivyo, Barçelona wanatarajiwa kuwatema wachezaji wengine wakubwa katika wiki zijazo kwa ajili ya kupunguza gharama.

Griezmann ni mmoja wa waliopata kipato kikubwa ndani ya Barçelona huku ikiripotiwa kuwa klabu hiyo wanaweza kumuuza Mfaransa huyo.