November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naseeb Abdul aka 'Dimond Platnumz'

Mambo mawili Diamond mbioni kuyafanya kipindi hiki

Kuipa Serikali Hoteli kwa ajili ya Karantini
Aeleza utaratibu wa kulipa kodi za nyumba 500

MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, ndivyo utakavyoweza kusema, kufuatia msanii wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media hapa nchini, Naseeb Abdul maarufu ‘Dimond Platnumz’ baada ya kuweka wazi kuwalipia kodi za nyumba kaya 500, katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Diamond amesema, atachangia ëkodi ya pangoí kwa kaya 500 nchini kwa ajili ya kupunguza makali ya kiuchumi kwa Watanzania katika kipindi hiki kigumu.

Akizungumzia hilo katika mahojiano na wasafi FM jana Diamond alisema, ameguswa na hali ya sasa, hivyo hana budi kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli kwani baadhi ya watu wamekwama kwenye biashara zao na suala la kodi ni changamoto kubwa.

“Najua katika kipindi hiki cha janga la Corona, mambo mengi hayapo sawa, hususani upande wa biashara, na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa magumu kwa watu wengi, miongoni mwa walioathirika na janga hili na mimi pia nimoî alisema Diamond.

Hata hivyo, msanii huyo ameweka wazi utaratibu wa kutoa fedha hizo ili kuhakikisha figisufigisu hazitakuwepo, kwa kutumia serikali za mitaa pamoja na timu yake ambayo itapita mitaani ili kuwafikia walengwa kama wamama wajane, walemavu na wale wote wenye mahitaji ya kweli.

Kwa upande wa Mikoani Diamond alisema, kila mkoa fedha hizo zitapewa familia tano na asilimia kubwa itakuwa Mkoa wa Dar es salaam.

“Maamuzi ya kusaidia watu yametokana na malezi niliyolelewa, maisha niliyotokea na historia yangu ya nyuma. Nikikumbuka shida nilizopitia , napata Moyo wa kusaidia Wengine,” alisema.

Mbali na hivyo, pia Diamond alisema, amenunua hotel ya kisasa yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Mikocheni B, na katika kipindi hiki cha janga la corona ataitoa kwa serikaali bure, kama mchango wake ili itumike kama karantini na kama itafaa itumika kama hospitali.

Alisema, hoteli hiyo inavyumba zaidi ya 30 ambayo itasaidia kusogeza huduma karibu kuliko mloganzila ambapo pana umbali kwa wakazi wengi hapa nchini.

Tanasha Dona

Tanasha Dona

Kuhusu kutengana na aliyekuwa mpenzi wake Tanasha Dona raia wa Kenya Diamond alisema, hajatengana na Tanasha kwasababu ya kufumaniana, bali kuna sababu ambazo yeye binafsi alimwambia na kusema anahitaji nafasi, hivyo aliheshimu maamuzi yake.

“Nilipanga kumuoa Tanasha 100% , kwasababu ni mwanamke ambae nilitulia Sana wakati nipo nae, niliweka ujana wangu pembeni lakini ndio hivyo kila kitu kinapangwa na Mungu,” alisema Diamond.

Hata hivyo Diamond alisema, walipokuwa Kigoma Tanasha alibadili Dini na kuwa Muisilamu jambo ambalo alimshukuru Sana Ricardo Momo ambaye ndio aliyefanikisha jambo hilo.

Diamond alisema, kufuatia kufanikisha jambo hilo la kumbadilisha Dini Tanasha alimuahidi Ricardo Momo kumpa Kiwanja

Hamisa Mobetto

Hamisa Mobeto

Akizungumzia juu ya Hamisa Mobeto kushiriki kwenye wimbo mpya wa Ali Kiba uitwao ‘Dodo’ Diamond alisema, yeye ndiye aliyetoa ruhusa Hamisa Mobetto ashirikiane kwenye wimbo huo ili kuongeza nguvu kwenye video ya DODO.

“Katika suala zima la muziki, si dhani kama kuna kitu kibaya, kwa wasanii kushirikiana, Ali Kiba anaweza kumpa sapoti Hamisa na yeye pia anaweza kufanya hivyo, kwa hiyo nilimpa baraka zote kushiriki wimbo wa ‘Dodo’,” alisema Diamond.

Ikumbukwe kua Diamond na Mobeto waliwahi kuwa wapenzi na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja aitwaye Dylan.

Zari Hassan

Zari Hassan

Akimzungumzia mzazi mwenzie Mfanyabiashara kutoka Uganda ambaye kwa sasa anaishi Afrika Kusini Zari Hassan maarufu ‘Zari thebosslady’, Diamond alisema, Baada ya kuona ule ujumbe wa Zari, alimpigia simu na kumueleza.

“Licha ya tofauti zetu, ila bado namuheshimu sana Zari. Alinielewa na nadhani baada ya janga la Corona kuisha tutapanga namna ya kuwalea watoto wetu,” alisema Diamond.

Baada ya Diamond kutangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa atatoa msaada wa kuwalipia kodi ya nyumba Kaya 500 hapa nchini, kama mchango wake kwa Serikali kutokana na janga la Corona.

Kufuatia kauli hiyo ya Diamond, Zari alitoa povu kuwa msanii huyo hajali watoto wake. Hajui wanakula nini /wanasoma vipi, Wanatibiwa vipi.

Zari alishangaa kwanini Diamond anataka kusaidia watanzania 500 kulipa kodi ikiwa familia haijali.