July 31, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama Ongea na mwanao kufanya Dua maalumu kwa wasanii waliopita

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

MWENYEKITI wa taasisi ya Ongea na Mwanao, Steve   Nyerere, kesho atawaongoza watanzania kwenye dua maalumu  ya kuwaombea wasanii, wachezaji na Waandishi wa habari waliotangulia mbele ya haki.

Steve amebainisha kwamba shughuli hiyo ya dua kwa wasanii waliotangulia mbele ya haki itaanza saa tatu asubuhi, itaongozwa na masheikh na wachungaji

Hayo amebainisha leo, Julai 31, 2026 jijini Dar es Salaam na kuwaomba watanzania kushiriki kwenye tukio  hilo linalojenga umoja kwa nchi na Taifa Kwa ujumla.

“Kesho tutawakumbuka makundi yote, ya wasanii, wachezaji, Waandishi wa Habari, viongozi  mbalimbali waliotangulia mbele ya haki,” amesema.

Pia kuelekea shughuli hiyo amewaasa vijana kwa makundi yote  kulinda amani ya Taifa kwa unyenyekevu na heshima  kubwa Kwa maslahi ya nchi.

Nyoshi El Saadat, naye amesema kuwa amesema jambo hili ni kubwa na la kupongeza na kuomba watanzania wote kujitokeza katika dua hiyo.

Abdallah Mkumbila, “Muhogo Mchungu”, amesema kuwa jambo la kuwaombea dua waliotangulia mbele ya haki ni jambo jema kwa maana Kwa maelezo ni kwamba pale kaburini hatujui palivyo,” amesema.

Ally Choki, kesho ni siku ya baraka kuwaombea ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki, naomba wote watnzania wajitokeze.
 
Andrew Sekidia, waliotangulia wametuachia amani ambayo inafanya hadi leo  tuendelee kufanya majukumu yetu vema , hivyo tuendelee kudumisha amani.

Salum Abdul  ‘Chiky’ ambaye ni mwenyekiti wa chama Cha Waigizaji Tanzania, amesema kesho wanakutana kwa ajili ya kuwaombea wenzatu, tunaamini hata malaika watakuwepo nawaombeni mfike kwa wingi.