December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama Kanumba amkumbuka mwanae

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

MAMA mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu Tanzania Steven Kanumba , Florah Mtegoa, amesema hatua ya wasanii kuandaa  tukio la kuwaenzi wasanii waliofariki limempa faraja kubwa hasa wakati huu wa miaka 12 ya kifo cha mwanaye Kanumba.

Flora ambaye pia amepoteza mtoto wake wa kiume Seth ambaye ni mdogo wake Kanumba, amesema ni kwa miaka mingi wasanii hawajawa na tukio kama hilo.

“Ninampongeza sana Steve Nyerere kwa kuandaa jambo hili la kuwaenzi wenzetu waliotangulia mbele za haki.Limenipa faraja kubwa ,”amesema.

Wasanii nchini leo wanafanya tamasha maalumu la kuwakumbuka wasanii, wanamichezo na watangazaji nyota waliofariki, katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.