Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
IMEELEZWA Vijana na wanawake nchini Tanzania, kama katika mataifa mengine ya Afrika , wanazidi kujiajiri kwa kufanya biashara mtandaoni kupitia simu za mkononi.
Akizungumza hivi karibuni nchini Kenya ,Meneja Mkuu wa kampuni ya QNET Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara Biram Fall,wakati wa
uzinduzi wa malipo ya fedha kwa njia ya simu kwa wawakilishi wao kwa nchini Tanzania, Kenya na maeneo mengine ya Afrika.
Amesema kati ya fursa hizi ni uuzaji wa moja kwa moja ya huduma za fedha kwa njia ya simu ambao nimfumo rahisi wa biashara unaohitaji mtaji mdogo.”Sekta ya uuzaji wa moja kwa moja barani Afrika leo iko katika hatua ya ukuaji na tasnia hii inakua kwa kasi kwa sababu ya kuongezeka kwa wajasiriamali wadogo wadogo,” amesema na kuongeza
“Kwa kweli ni vigumu kupata kampuni inayofanya biashara ya moja kwa moja barani Afrika ambayo haina kipengele cha malipo kwa njia ya simu, hivo na sisi sasa tumezindua malipo kwa njia simu kusaidia kukuza biashara za wa wakilishi wetu,” ameeleza
Amesema Mfumo wa biashara za moja kwa moja unatoa ajira nyingi kutoka na mtaji wake kuwa mdogo.
Amesema kwa upande mwingine, uuzaji wa moja kwa moja unakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa biashara ya mtandaoni Afrika.
Fall amesema katika ripoti ya McKinsey inaonyesha kuwa thamani ya soko la mtandaoni Afrika itafikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni 2.1 ifikapo mwaka 2025.” Ripoti hiyo pia inasema, kwa sasa, zaidi ya asilimia 40 ya Waafrika wote wanaweza kupata aina fulani ya mtandao jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa huduma za mtandaoni,”amesema na kuongeza
“Suala lingine lililo pelekea kuongezeka kwa biashara za mtandaoni ni janga la uviko 19,” amesema Fall.
Amesema katika kipindi cha uviko 19 watu wengi walizuiiwa kusafiri hivo kuanza kufanya biashara mtandaoni badala ya kukutana uso kwa uso.
“Janga hilo lilifanya wasambazaji na wateja kutegemea shughuli za biashara ya kielektroniki ili kukidhi mahitaji yao ya bidhaa,”amesema
Aidha amesema kwa kuzingatia maendeleo haya, kampuni ya QNET, moja ya kampuni kubwa za biashara ya moja kwa moja sasa imezindua malipo kwa njia ya simu.
Amesema faida kubwa ya kutumia malipo kwa njia ya simu ni urahisi wakuwafikia wateja na kupunguza usumbufu wa kwenda benki au madukani kununua bidhaa.
“Kwa kuanzishwa malipo kwa njia ya simu, QNET inataka kurahisisha ufanyaji wa kazi kwa wasambazaji wake na kuwasaidia kukuza biashara zao,” amesema.
Kampuni hio imezindua malipo kwa njia ya simu katika nchini Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, na Ghana na inapanga upanuzi zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati