January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Malikia Elizabeth II awatakia England kila la Kheri

LONDON, England

TIMU ya Taifa ya England chini ya Kocha wake Gareth

Southgate imepokea ujumbe kutoka kwa Malkia Elizabeth

II, kabla ya mchezo wao wa Fainali ya Euro 2020 dhidi

ya Italia leo, majira ya saa 4:00 usiku.

Akipokea ujumbe huo, Katika mkutano wake na waandishi

wa habari kabla ya mechi, Southgate amesema; “Tumepokea

barua ya kututakia kila la heri kutoka kwa Malkia na

Waziri Mkuu kwenda kwa timu nzima na kutambuliwa kwa

wachezaji na wafanyakazi wote.

England imefika Fainali ya Euro kwa mara ya kwanza,

baada ya miaka 55, tangu kuingia katika fainali ya

mashindano makubwa na kufanya hivyo walivyotwaa Kombe

la Dunia mwaka 1966 .

Malkia Elizabeth II alihudhuria siku hiyo, wakati

England ikiifunga Ujerumani Magharibi mabao 4-2 kwenye

Fainali ya Kombe la Dunia 1966.