December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu

Makusanyo ya fedha za semina kumewezesha kujenga vituo vya afya’

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa makusanyo ya fedha za semina na makongamano kumewezesha Wizara ya Afya kupata bajeti ya sh Bil.7 kujenga vituo vya afya nchi nzima.

Ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi mara baada ya kufungua huduma ya dharura ya upasuaji kwa mama mjamzito Katika kituo Cha afya Mikanjuni Jijini Tanga.

Waziri Ummy amesema kuwa fedha hizo zimeweza kusaidia kusogeza huduma bora za afya karibu na wananchi tofauti na hapo awali.

“Kwa kweli namshukuru Rais Magufuli kwa kukubali fedha hizo kuzielekeza Katika ujenzi wa miradi ya vituo vya Afya ambavyo vimeweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi hasa wa hali yachini”amesema Waziri Ummy.

Aidha Mganga Mkuu wa kituo Cha Mikanjuni Dkt.Mwajame Bausy amesema kuwa jumla ya vituo vyaafya vitatu vimeweza kuanza kutoa huduma ya dharura kuanza Juni mwaka huu.

“Tayari wajawazito 5 katika kituo Cha afya Makorora na 3 katika kituo Cha afya Ngamiani wameweza kupata huduma ya upasuaji wa dharura na hivyo kupunguza msongamano katika hospitali ya Rufaa ya Bombo”amesema Dkt. Bausy.