Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa, imeweka onesho adimu la vioneshwa vya urithi wa asili na utamaduni ndani ya viwanja vya Bunge, kupitia gari Maalum, kwa lengo la kuelezea Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo kupitia Taasisi ya Makumbusho.
Akikagua maonesho hayo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ameipongeza Idara ya Malikale kupitia Taasisi ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania kwa ubunifu makubwa wa Makumbusho hiyo inayotembea.

Kairuki ameagiza hamasa ifanyike zaidi hasa kwenye maonesho hayo ili Waheshimiwa Wabunge waweze kushirikiana na Makumbusho, kuwafikishia maonesho hayo ya Kimakumbusho wananchi kwenye maeneo yao.

Aidha, katika kuelekea uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya Mwaka 2023/2025, Wizara hiyo imeweka maonesho mbalimbali hususan ya Wanyama hai, Makumbusho inayotembea, nyama choma za Wanyamapori , kwenye viwanja vya Bunge ambayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa Waheshimiwa Wabunge na wagani mbalimbali wanaofika Bungeni.
More Stories
Waziri Silaa ashiriki kupandisha vifaa ujenzi wa Mnara wa mawasiliano Idete
Waziri Silaa aelekeza Minara yote 758 kuwashwa ifikapo Mei 12,2025
Wananchi Vunjo watatua kero ya barabara,wataka zahanati yao