January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makonda amtembelea Mama yake Magufuli

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Komredi Paul Makonda akiendelea na ziara yake katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa amefika kumsalimia Bibi Suzana Magufuli ambaye ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, Nyumbani kwake Chato mkoani Geita

Makonda anaendelea na ziara ya aina yake katika mikoa ya Kanda ya ziwa inayobeba malengo kadhaa kama vile kujitambalisha kwa wananchi na wanachama wa CCM katika mikoa hiyo lakini pia kutatua kero za wanyonge papo kwa papo.