May 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makonda amtaka Mwigulu kuifafanulia serikali mikopo kausha damu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amemtaka Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kueleza umma juu ya kauli ya Serikali kuhusiana na malalamiko juu ya Mikopo maarufu kama kausha damu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Mwenezi Makonda kupokea kero hiyo na kuamua kumuuliza maswali 3 Waziri wa fedha kwa niaba ya Wananchi, mawasli hayo ni;
1 Je? Kausha damu wana leseni?
2 Na kama wanazo anayepiga mahesabu ya riba ni nani?
3 Kwenye riba yao Serikali inanufaika vipi?

Hayo yanejiri wakati Mwenezi Makonda akizungumza na Wananchi wa Singida kwenya Mkutano wa Hadhara uliofanyika jana tarehe 25 Januari, 2024 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.

Katika kutoa ufafanuzi jambo hilo, Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba amesema kuwa ni kweli serikali walitoa leseni lakini riba ilikuwa ni kwa utaratibj wao si wizara wala Waziri wanaopata chochote lakini ndio ya kipindi cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuondoa usumbufu wanaopata wananchi kwa kumuelekeza Gavana wa Benki kuu na idara ya mikopo ndani ya Wizara ya fedha kupitia upya masharti ya vibali kwa leseni hizo na kuweka upya utaratibu mzuri.

Pia, amebainisha kuwa hadi sasa kilichofanyika ni kupitia upya leseni hizo na kuweka utaratibu mzuri na ambapo kilichofanyika ni leseni kutoa masharti ya wigo uliopo kama kwenye mabenki ili kuepukana na uholela unaoendelea.

Vilevile, Waziri Mwigulu amesema tayari Serikali imedhafuta leseni holela kwasababu ya uwekaji wa masharti ya riba kubwa na unyanyasaji na kubainisha kuwa wengine walikuwa hadi na mahabusu zao za kimyakimya.

Aidha, Waziri Mwigulu ametoa rai kwa Watanzania wote pale ambapo kutakuwa na watoa mikopo hao maarufu kausha damu kutokana na tabia zao za ukiukwaji wa taratibu na masharti ya serikali basi wasisite kutoa taarifa katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Serikali itawafutia leseni zao mara moja.