Na mwandishi wetu
MAKANDARASI nchini wametakiwa kuisoma mikataba kwa umakini mkubwa kabla ya kuisaini ili kuepuka kuingia kwenye mikataba ambayo wanaweza kushindwa kuitekeleza na kukimbia miradi wakati wa kuitekeleza.
Hayo yamesemwa Disemba 1 , 2021 Jijini Da es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Consolata Ngimbwa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi kuhusu usimamizi wa mikataba.
Mhandisi Ngimbwa amesema ni vyema mkandarasi akajiridhisha na mkataba anaoingia kwa kuusoma vizuri na kama haelewi kuomba ufafanuzi ili asijiingize kwenye mkataba ambao hataweza kuutekeleza.
” haya mafunzo ya usimamizi wa mikataba ni muhimu sana hivi ndo muhimu ambavyo unatakiwa kuviangalia pale unapopewa mkataba wako wa kazi kabla ya kusaini ili mkataba uwe na faida kwa pande zote mbili kati ya mkandarasi na mteja wako ” amesema Mhandisi Ngimbwa
Aidha amewataka makandarasi kuacha tabia ya kusaini mikataba bubu bila kujua namna watakavyofanya kazi huku akikemea tabia ya Makazi kufanya kazi bila malipo ya awali (Advance payment) .
” Kama usione sehemu hujaelewa usijifungie ndani uliza watu wakuelekeze kuna wataalamu wapo na hiyo ndo kazi yao ni bora ukauliza ili kuepekuka tatizo la kusaini mikataba bubu” amefafanua Mhandisi Ngimbwa
Nao baadhi ya Makandarasi waliopatiwa elimu hiyo wamesema mafunzo hayo yatakuwa na tija katika taaluma yao haswa katika suala la usimamizi wa mikataba huku wakitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili katika tasnia yao ikiwepo ucheleweshwaji wa malipo pamoja na uhaba wa kazi.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti