January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa Rais wa Marekani ahitimisha ziara yake nchini Tanzania

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango wakati akiwaaga wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania leo tarehe 31 Machi 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango akimuaga Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na Mumewe Douglas Emhoff katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 31 Machi 2023 mara baada ya kuhitimisha ziara nchini Tanzania.