December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar,Othman Masoud Othman aifariji familia ya Marehemu Maalim Seif

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Zanzibar

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, Leo Jumapili Oktoba 8, 2023 amefika Langoni- Maungani, Wilaya ya Magharibi B Unguja, kwaajili ya Kuwafariji na Kutoa Mkono wa Pole kwa Wanafamilia wa Mzee Ismail Sharif, Kaka wa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Kifo cha  Hasnuu Ismail Sharif (68), aliyefariki-dunia Usiku wa Kuamkia Jumamosi ya jana, hapo Nyumbani kwao Langoni-Maungani, baada ya kuugua kwa Majuma kadhaa.

Marehemu Hasnuu ambaye amewacha Mke na Watoto Watatu (3), pia amezikwa jana katika Makaburi ya hapo-hapo Langoni-Maungani, kisiwani Unguja.