Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, Leo Jumatatu Septemba 02, 2024, amewasili Kisiwani Unguja, akitokea Arusha Tanzania Bara, baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili (2) mkoani humo.
Katika Ziara hiyo, ambayo iliyojumuisha shughuli mbali mbali za serikali na jamii, pia alishiriki uzinduzi, akiwa Mgeni Rasmi, wa Mbio Maalum za Marathon Kwaajili ya Watoto Wenye Tatizo la Midomo-Wazi (Clefts), na Kilele cha Maadhimisho ya Miaka Kumi (10) ya Taasisi ya ‘The Same Qualities Foundation (SQF)’.
Akiwa Uwanja wa Ndege wa Kisongo jijini Arusha, Othman amesindikizwa na viongozi mbali mbali wa serikali na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha- Mjini, Felician Gasper Ntahengerwa.
More Stories
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao
Dkt.Kafumu:Uteuzi wa Rais Samia umezingatia katiba
Kliniki ya sheria bila malipo yazinduliwa Kilimanjaro