January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ashiriki mazishi ya Jokha

Na Haji Mtumwa, TimesMajira Online, Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Alhaj  Othman Masoud Othman, leo amejumuika na Viongozi na wananchi mbalimbali katika Maziko ya Shangazi wa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban.

Marehemu Bi. Jokha Ali Salim, alifariki dunia jana Juni 25, katika Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja na kuzikwa leo Juni 26, katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi, Amin!