December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamba kutimiza ndoto ya Rais Samia LNG

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Moja kati ya mambo makubwa kwenye #BajetiYaNishati ni utekelezaji wa mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG). Maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo yataanza katika mwaka ujao wa fedha.

Wabunge, Salma Kikwete (Mchinga) Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), Katani Katani (Tandahimba), Elibariki Kingu (Singida Magharibi) kwa nyakati tofauti wamempongeza Waziri January Makamba kama msaidizi wa Rais katika sekta ya Nishati kwa kufufua mazungumzo ya mradi huo na sasa ndoto ya Rais inakwenda kutimia.

Kwa miaka takriban 8, majadiliano juu mradi huo yalikwama, lakini sasa Wizara ya Nishati chini ya Waziri Janaury Makamba kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu imeweza kufufua majadiliano hayo.