January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi

Na Mwandishi wetu

Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla ameyasema hayo akizungumza na Viongozi na Wanachama wa Wilaya ya Kigamboni ikiwa ni muendelezo wake wa kuzungumza na Wanachama na viongozi wa Mkoa wa Dar es salam.

“Nimesikia klipu moja kiongozi wa Chadema sijui huko Mpanda anatoa taarifa kwamba CCM imesimamisha wagombea kila sehemu sisi tumeshindwa anaulizwa mkakati wenu nini anasema yale maeneo ambayo hatukusimamisha Wagombea tutawafanyia fujo wake”

CPA Makalla amesisitiza CCM kwenye Uchaguzi huu itafanya kampeni za kistaarabu kwa kutumia 4R za Dkt Samia lakini Uchaguzi huu hatuhitaji fujo tutofautiane kiitikadi lakini Tanzania baada ya Uchaguzi ibaki moja ,salama na wamoja